Roboti Ni Nini?

Kwenye posti yangu iliyopita ambayo ni ya kwanza. Niliandika kuhusu “ajira kuchukuliwa na roboti”. Hivyo Leo nimeona nikueleweshe roboti ni kitu gani haswa?. Endelea kusoma hadi mwisho!.

Roboti ni kifaa cha kielektroniki chenye uwezo wa kimakenika, kinachotumika kufanya yaliyo nje ya uwezo wa binadamu. Japo kifasihi roboti ni sawa na mtumwa.

Roboti hutumia mitambo na programu maalumu kuiongoza. Roboti za siku hizi zinauwezo wa kufanya kazi kwa kujitegemea. Hazihitaji tena uongozwaji wa moja kwa moja mfano kwa kubonyeza kitufe au kutumia sauti

Roboti yawezakuwa imeundwa aidha kwa chuma au mwili wa kawaida. Na baadaye kuwekewa akili bandia. Wengi tumezoea kuona zile za chuma kwenye sinema. Na hatujazoea kuona zenye muundo kama huu, hapa chini.

Roboti zinafanya kazi lukuki duniani. Na kila siku zinazidi kuongezeka, kama uhudumu hotelini,viwandani na hata safari za nje ya dunia. Kwa miaka 5-10 ijayo roboti zitakuwa ni sehemu ya maisha yetu.

Roboti hutengenezwa ili kufanya kazi moja tu,ila kwa ufanisi wa halo ya juu. Roboti hutegemea vifaa viitwavyo microprocessor.  Ili kutimiza kazi yake. Kifaa hiki ndio hutumika kama ubongo kwa roboti. Kifaa hicho (microprocessor) ndicho hutoa majibu roboti ifanye mini, kulingana na mazingira yake.

Ubora wa roboti hupimwa na wingi wa vipengele/vifaa vyake. Kama mikono/viungio vingi, microprocessor nyingi. Hizi ni baadhi tu ya viashirio vya roboti. Mwenye utendaji kazi wa hali ya juu.

Kwenye posti inayofuata nimeeleza kiundani matumizi ya roboti. Nikiambatanisha na picha zake.

Leave a comment